Joshua 19:1-8

Mgawo Kwa Simeoni

1 aKura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda. 2 bUlijumuisha:

Beer-Sheba (au Sheba), Molada,
3 cHasar-Shuali, Bala, Esemu, 4Eltoladi, Bethuli, Horma, 5Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa, 6Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.
7Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake, 8pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii mpaka Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni ukoo kwa ukoo.
Copyright information for SwhNEN